Mikakati ya tume ya maadili na kupambana na ufisadi

  • | K24 Video
    1 views

    Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC inakusudia kuandama kesi ndogo ndogo za ufisadi inazosema zinatumiwa kufuja mamilioni ya pesa na viongozi wakuu serikalini. Ikiwa ni mwaka mmoja sasa tangu Rais William Ruto kuchukua usukani, mawaziri na viongozi wakuu serikalini vilevile wanamulikwa katika kile kinachoonekana kubadilika ghafla kwa maisha yao kwani baadhi wamenunua majumba ya kifahari, magari na hata saa ya thamani ya shilingi milioni thelathini na saba.