MIkasa ya moto

  • | Citizen TV
    2,415 views

    Mtazamaji polisi wanachunguza kiini cha moto uliozuka eneo la 56 Kawangware Ijumaa usiku baada ya lori la mafuta ya petroli, lililokuwa limeegeshwa kujaza mafuta kwenye kituo cha eneo hilo, kulipuka na kusababisha majeraha kwa wapangaji kadhaa. Aidha, kwenye tukio jingine la mkasa wa moto, polisi pia wanachunguza chanzo cha moto ulioteketeza jengo la kihistoria la Limuru country club kaunti ya Kiambu.