Milima ya Wundanyi yawavutia watalii kaunti ya Taita Taveta

  • | Citizen TV
    859 views

    Msimu huu wa likizo umeendelea kuwavutia watalii maeneo mbalimbali nchini huku baadhi wanaozuru kaunti ya Taita Taveta wakipendezwa na milima iliyo kaunti hii. Kaunti hii ya Taita Taveta ni mojawapo ya maeneo yaliyo na mandhari ya kupendeza haswa maeneo ya Wundanyi ambayo milima mirefu zaidi imeendelea kuwavutia watalii.