Mimea ya bangi iliyopandwa nyumbani yanaswa Elgon View mjni Eldoret

  • | Citizen TV
    250 views

    Maafisa wa polisi mjini Eldoret wamenasa bangi yenye thamani ya shilingi million 1.5 kwenye nyumba moja ya kibinafsi mjini humo. Bangi hiyo ilipatikana ikiwa imepandwa kwenye nyumba hiyo iliyo kwenye mtaa wa kifahari wa Elgon View. Naibu kamanda wa polisi katika kaunti ya Uasin Gishu Zacchaeus Ngeno amesema kuwa wanaendeleza uchunguzi kubaini washirika wa biashara hiyo haramu. Kwa sasa, Ng'eno anasema wameendeleza msako wa kumtafuta mshukiwa ambaye alitoweka. Aidha ameonya kuwa wako ange kukabiliana na mtu yeyote anayeshiriki biashara haramu ya aina hii