'Mimi si kama Dangote lakini ningemjengea mamangu mtaa mzima'

  • | BBC Swahili
    Akiwa na umri wa miaka 10 tu mchekeshaji Emmanuella Samuel ametumia mapato yake aliyoyatengeneza kupitia mtandao wake wa You Tube kuwajengea wazazi wake nyumba. Amekuwa nyota katika chaneli ya You Tube maarufu ya mchekeshaji Mark Angel, tangu alipokuwa na umri wa miaka mitano. Akimshukuru mama yake Emmanulla amesema mama yake anafaa kupewa nyumba nyingi. Je , wewe umemfanyia nini mzazi wako? #bbcswahili #nigeria #sanaa