Mjadala kuhusu makato ya nyumba

  • | K24 Video
    155 views

    Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula amewasilisha ilani ya rufaa katika mahakama ya juu ya kutaka kubatilishwa kwa uamuzi wa mahakama ya rufaa ,unaoizuia serikali kukusanya ushuru wa nyumba kutoka kwa waajiriwa. Hili likijiri chama cha walimu wa shule za upili kenya , KUPPET, Kinaitaka serikali irejesha makato ya ushuru wa nyumba ambayo yamelipwa kwa niaba ya wanachama wa chama hicho kufuatia uamuzi wa mahakama uliotangaza ushuru huo kuwa kinyume cha katiba