Mkanda wa Video ukiwaonyesha Wapalestina waliokuwa chini ya ulinzi wakiwa wamevuliwa nguo

  • | VOA Swahili
    386 views
    Mkanda wa video ukiwaonyesha wanaume wa Kipalestina waliokuwa chini ya ulinzi wakiwa wamevuliwa nguo zote na kubakishwa na chupi huko Gaza, wakikalishwa chini na vichwa vyao kuinamishwa/ wanajeshi wa Israeli wamekusanyika karibu ya watu hao waliowekwa chini ya ulinzi. "Tunazungumzia watu binafsi waliokamatwa huko Jabalia na Shejaiya (huko Gaza City), kwenye ngome ya Hamas na vituo vya kimkakati,“ Msemaji wa serikali ya Israeli Eylon Levy aliweleza waandishi alipoulizwa kuhusu picha hizo za Wapalestina. “Tunazungumzia kuhusu umri wa wanaume wapiganaji ambao waliogunduliwa katika maeneo ambayo raia walitakiwa wawe wameondoka wiki kadhaa zilizopita. Jeshi la Israeli limekuwa likiwataka raia waondoke katika maeneo ambayo ina mipango ya kuendesha operesheni yake baada ya kuanzisha kampeni yake ya kuwatokomeza Hamas huko Gaza kufuatia kikundi cha wanamgambo wa Kiislam kufanya mauaji ndani ya Israel Oktoba 7," alisema. Husam Zomlot, mkuu wa Ubalozi wa Palestina huko London, alisema kwenye mtandao wa X inaonyesha “ubinadamu unapitia kipindi cha giza nene katika historia. Mwanasiasa wa Palestina Hanan Ashrawi alisema katika mtandao wa X tukio hilo ni “jaribio la kitendo cha kuwadhalilisha na kuwanyanyasa wanaume wa Kipalestina … walivuliwa nguo na kuonyeshwa kama ushindi wa vita”. - Reuters #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #hospitali #Nasser #wagonjwa #madawa