Mkandarasi adai kuhangaishwa na maafisa wa kaunti ya Mombasa kuhusu malipo ya ada ya saruji

  • | Citizen TV
    326 views

    Kizaazaa kilizuka baina ya mkandarasi mmoja anayehusika na ujenzi wa barabara kuu ya Mombasa - Malindi na maafisa wa serikali ya kaunti kuhusu ulipaji wa ada ya saruji inayotumika katika ujenzi wa barabara hiyo. Kulingana na maafisa wa kaunti, mkandarasi huyo anapaswa kulipa ada ya shilingi 3,400 huku mkandarasi huyo akidai kuwa yuko na stakabadhi zote na kudai kuhangaishwa na maafisa hao zaidi ya mara moja wakidai hongo.