Mkazi wa mji wa Derna, Libya aeleza jinsi bwawa lilivyopasuka na wakashtukizwa na mafuriko

  • | VOA Swahili
    1,067 views
    Mkazi wa mji wa Derna, nchini Libya Mustafa Salem aeleza janga hilo lilivyotokea: “Baadaye tukasikia (bwawa) limepasuka na (maji) yameshafurika katika eneo. Watu walikuwa wamelala, hakuna aliyekuwa tayari kukabiliana na hali hiyo. Lakini hiki ndiyo kilichotokea – tutafanya nini. Kwangu mimi, nyumba yangu iko karibu na bonde, mkabala na Msikiti wa Al-Sahaba- familia yote inaishi karibu na kila mmoja, sote sisi ni majirani. Tumepoteza watu 30 hadi hivi sasa, watu 30 wa familia moja. Hatujaweza kumpata yeyote kati yao.” #Libya #RedCross #redcrescent #voa #voaswahili - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.