'Mke hakupaswa kuendelea kuwahudumia wagonjwa wa Covid19 akiwa na mimba ya miezi 7. Sasa amefariki'

  • | BBC Swahili
    Mume azungumzia machungu ya kumpoteza mke wake aliyekuwa mjamzito kwa virusi corona. Mary alikuwa muuguzi katika hospitali moja Bedfordshire, Uingereza. Alipatikana na virusi vya corona mapema Aprili na kufariki wiki moja baadae. Madaktari walifanikiwa kumtoa mtoto kwa njia ya upasuaji lakini mume wake, Ernest, anasema hakustahili kufanya kazi kuanzia mwanzoni mwa janga la corona kwasababu alikuwa mjamzito kiasi cha kuwa tayari kujifungua muda wowote. Hatahivyo Hospitali ya Bedfordshire imesema inachunguza kisa hicho: "Tumesikitishwa na kifo cha Mary." #covid19 #mtoto #Mjane