Mkurugenzi wa hospitali ya Gaza European akiwapokea madaktari bingwa kutoka Marekani

  • | VOA Swahili
    476 views
    Timu ya madaktari wa upasuaji wa kimataifa wametembelea hospitali yenye msongamano wa wagonjwa huko Khan Younis Jumanne (Desemba 26), wakati walipowasili Gaza kuwasaidia madaktari wa eneo kuendelea na upasuaji mgumu. Ujumbe huo, ambao unawawakilishi kutoka shirika la “Rahma Worldwide,” taasisi ya hisani isiyokuwa ya kibiashara ya Islamic yenye makao yake Marekani, inajumuisha wataalam sita wa upasuaji. Akram Adel Moushtahi, msemaji wa ujumbe wa “Rahma Worldwide’ unaotembelea European Hospital, alisema madaktari ulimwengu mzima wako tayari kuja katika eneo hili lililozingirwa kusaidia, hususan wale ambao wanaweza kufanya upasuaji, lakini wanataka waruhusiwe kuingia Gaza. Asilimia 20 tu ya hospitali huko Ukanda wa Gaza zinafanya kazi na zote zimeelemewa, alisema Mtaribu wa Timu ya Madaktari wa Dharura wa Shirika la Afya Duniani huko kusini mwa Gaza Jumanne. Jumla ya Wapalestina 21,110 wameuawa na wengine 55,243 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Israeli huko Gaza tangu Oktoba 7, wizara ya afya Gaza ilisema Jumatano. Idadi hiyo inajumuisha Wapalestina 195 waliouawa na 325 waliojeruhiwa katika kipindi cha saa 24, wizara hiyo imeongeza. - Reuters ⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #GadiEizenkot #wazirimkuu