Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji atarajiwa kupigwa msasa leo

  • | Citizen TV
    148 views

    Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji anatarajiwa kupigwa msasa leo kufuatia uteuzi wake kuwa mkuu wa idara ya ujasusi nchini. Noordin atapigwa msasa na kamati ya bunge la kitaifa kuhusu ulinzi na maswala ya ujasusi na mashauri ya kigeni. Noordin anapigwa msasa huku kukiwa na tetesi na pingamizi kuhusu uteuzi wake. Baadhi ya mashirika ya kijamii yamepinga uteuzi wa Noordin kuwa mkuu wa ujasui. Kamati ya bunge inayoongozwa na mbunge wa Belgut Nelson Koech inatarajiwa kumuhoji Noordin baadaye adhuhuri