Mkurugenzi wa NIS Noordin Haji asema hakuna vifaa vya ulinzi vya kutosha

  • | Citizen TV
    1,068 views

    Mkurugenzi wa Idara ya ujasusi Nurdin Haji, ameonya kuwa upungufu wa bajeti unaweza kudhoofisha juhudi za usalama wa taifa. Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ulinzi Bungeni, Haji amesisitiza kuna haja ya kufadhili kikamilifu vyombo vya usalama vinavyolinda nchi. Idara ya Ujasusi NIS, ambayo imepewa Shilingi bilioni 55 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 inaonya kuwa fedha hizo hazitoshi na upungufu huo unahatarisha vyombo vya usalama vinavyokabiliana na vitisho vipya kama uhalifu wa mtandaoni na pia ugaidi. NIS ilikuwa imeomba shilingi bilioni 65 katika bajeti..