Mkutano wa COP27: Afrika inataka nchi tajiri kufadhili miradi ya kuokoa mazingira

  • | VOA Swahili
    198 views
    Mkutano wa Hali ya Hewa: Moja ya matarajio makubwa ya nchi za Afrika ni kupatiwa fedha zilizoahidiwa na mataifa tajiri katika mikutano iliyopita ili waweze kugharimia miradi itakayopunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa haraka iwezekanavyo. Mwandishi wetu anachambua athari kubwa inayozikabili nchi za Kiafrika. Endelea kusikiliza repoti hii maalum ya mkutano wa kimazingira wa COP27, unaofanyika Sharm EL-Sheikh.... - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.