Mkutano wa ulinzi wa mazingira wafikia maazimio Kigali, Rwanda

  • | VOA Swahili
    1,909 views
    Je, mashirika na jumuiya za watu wa kiasili wanapokea ufadhili uliowekezwa barani afrika? Je kutakuwa na afueni katika kongamano la maeneo yaliyolindwa APAC, Na kama anavyoripoti mwanahabari wetu Hubbah abdi kutoka Kigali Rwanda katika kongamano linaloendelea la APAC mashirika ya kijamii yanatatizika kukuza au kuongeza fedha zao kwa sababu ya vizuizi vilivyojengwa ndani na changamoto katika jinsi yanavyofadhiliwa. PKG: Mombasa Chef Kutambuliwa kwa Kiswahili kama lugha moja ya lugha muhimu duniani kumeanza kuonyesha faida zake huku wajasiria mali mbali mbali wakitumia fursa hiyo kujiendeleza kutangaza na kuuza tamaduni za waswahili. Ripota wetu wa Mombasa Salma Mohamed amemfuatilia mpishi mchekeshaji jamilla Kizondo ambaye anatumia Kiswahili katika biashara za vyakula vya kitamaduni akiwa Marekani, Sasa yuko nyumbani Kenya!. PKG: DRC Business Mjini Goma kivu Kaskazini wakazi wanaomba suluhisho kuhusu mzozo kati ya DRC na Rwanda na tatizo la wapiganaji wa M23 ambao wamesababisha maisha kuwa magumu kutokana na mpaka kati ya Uganda na DRC kufungwa tangu waasi waudhibiti mji wa Bunagana. Mwandishi wetu wa DRC Austere Malivika ana ripoti zaidi. PKG: Sports: Basi ikiwa ni siku ya Ijumaa, mwanamichezo wetu Idd Ligongo ametukusanyia yale yanayoendelea viwanjani