Mkuu wa Majeshi Francis Ogolla kuzikwa Jumapili kulingana na alivyousia

  • | K24 Video
    160 views

    Familia ya mkuu wa majeshi jenerali Francis Ogolla imetangaza kuwa jenerali huyo atazikiwa jumapili kulingana na alivyousia. Kulingana na familia, Ogolla hakutaka mazishi yake yakawie siku nyingi na hivyo alitoa muda wa sa sabini na mbili. Hayo yakifahamika, wingu la simanzi liligubika nyumbani kwake eneo la usonga baada ya taarifa ya tanzia kutolewa kuhusu kifo cha Francis Ogolla na Sajini Cliffones Omondi miongoni mwa wengine kutangazwa. Hafla ya kijeshi ya kumpa mkono wa buriani Jenerali Ogolla itaandaliwa kesho jijini Nairobi.