- 21 viewsRais wa Kenya William Ruto Alhamisi jioni alitangaza kifo cha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Francis Ogolla, kilichotokana na ajali ya helikopta iliyotokea majira ya alasiri Kaskazini Magharibi mwa nchi. Akihutubia wanahabari katika ikulu ya Nairobi, Ruto alisema kuwa ndege hiyo ya kijeshi ilianguka eneo la Sindar kaunti ya Elgeyo Marakwet mwendo wa saa nane na dakika 20 alasiri. Ruto alisema watu wengine 9 pia walifariki katika ajali hiyo na kuongeza kwamba maafisa wengine wawili waliokuwa kwenye ndege hiyo walinusurika na wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini. Tisa hao ni pamoja na Brigedia Swale Saidi, Kanali Duncan Keittany, Luteni Kanali David Sawe, Meja George Benson Magondu, Kapteni Sora Mohamed, Kapteni Hillary Litali, Sajenti Mwandamizi John Kinyua Mureithi, Sajenti Cliphonce Omondi, na Sajenti Rose Nyawira. "Nina huzuni kubwa kutangaza kwamba Jenerali Francis Omondi Ogolla, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, amefariki” Rais Ruto alisema. Katika taarifa yake, Ruto alisema Ogolla aliondoka Nairobi Alhamisi asubuhi kuelekea kazini katika eneo la Bonde la Ufa, ambako alikagua ukarabati wa shule tano Elgeyo Marakwet. Pia alikuwa Turkana ambapo alikutana na kuzungumza na wanajeshi waliotumwa huko kabla ya kwenda Pokot Magharibi. Wakati wa ajali hii, Jenerali Ogolla na timu yake walikuwa wakielekea Kaunti ya Uasin Gishu. Kufuatia kifo cha Ogolla, Ruto ametangaza siku tatu za maombolezo huku bendera zikipepea nusu mlingoti. "Wakati huu wa maombolezo ya kitaifa, bendera ya Kenya, Bendera ya Jeshi la Ulinzi la Kenya, na bendera ya jumuiya ya Afrika Mashariki zitapepea nusu mlingoti katika balozi za Jamhuri ya Kenya na Kenya nje ya nchi," Ruto alisema. Uchunguzi umeanza kubaini kilichosababisha ajali hiyo. #mkuuwamajeshi #Jenerali #FrancisOgolla #rais #kenya #williamruto #ndege #jeshi #ajali #nairobi #voa #voaswahili
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Francis Ogolla Afariki katika Ajali ya Ndege
- 8 Jul 2025 - Deputy President Kithure Kindiki has said the government is enhancing partnerships with global technology companies to create more job opportunities for the youth.
- 8 Jul 2025 - The government has launched a fresh crackdown targeting foreign nationals from Burundi, Rwanda, the Democratic Republic of Congo (DRC), and Uganda’s Wagisu community residing in West Pokot County, over suspected involvement in cannibalism and human organ…
- 8 Jul 2025 - 36 suspects were arraigned on Tuesday at the Eldoret law court with charges of being in possession of weapons in public contrary to section 88 of the penal code.
- - DPP approves terrorism charges against Kawanjiru, Thiga, 35 others over June 25 chaos
- 8 Jul 2025 - The Cabinet Secretary for Health, Aden Duale, has vowed to end the practice of bed-sharing among patients in public health facilities to promote quality healthcare across the country.
- 8 Jul 2025 - Prime Cabinet Secretary Musalia Mudavadi on Tuesday, July 8, 2025, held a closed-door meeting with Central Organisation of Trade Unions (COTU) Secretary General Francis Atwoli. The meeting, which took place at Mudavadi’s office, focused on key national…
- 8 Jul 2025 - A sombre mood engulfed Ndumberi village in Kiambu County on Monday, July 7, after it emerged that 12-year-old
- 8 Jul 2025 - Kenya Simbas overcame a determined Uganda Rugby Cranes side with a 32-24 victory in the Rugby Africa Cup quarterfinals, booking their spot in the semifinals of the continental tournament. The fierce East African derby lived up to expectations as both…
- 8 Jul 2025 - Despite no means of autism detection during pregnancy, the signs can be observed in a child after birth
- 8 Jul 2025 - The suspects also face additional counts of arson and malicious damage to property.