- 995 viewsRais wa Kenya William Ruto Alhamisi jioni alitangaza kifo cha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Francis Ogolla, kilichotokana na ajali ya helikopta iliyotokea majira ya alasiri Kaskazini Magharibi mwa nchi. Akihutubia wanahabari katika ikulu ya Nairobi, Ruto alisema kuwa ndege hiyo ya kijeshi ilianguka eneo la Sindar kaunti ya Elgeyo Marakwet mwendo wa saa nane na dakika 20 alasiri. Ruto alisema watu wengine 9 pia walifariki katika ajali hiyo na kuongeza kwamba maafisa wengine wawili waliokuwa kwenye ndege hiyo walinusurika na wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini. Tisa hao ni pamoja na Brigedia Swale Saidi, Kanali Duncan Keittany, Luteni Kanali David Sawe, Meja George Benson Magondu, Kapteni Sora Mohamed, Kapteni Hillary Litali, Sajenti Mwandamizi John Kinyua Mureithi, Sajenti Cliphonce Omondi, na Sajenti Rose Nyawira. "Nina huzuni kubwa kutangaza kwamba Jenerali Francis Omondi Ogolla, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, amefariki” Rais Ruto alisema. Katika taarifa yake, Ruto alisema Ogolla aliondoka Nairobi Alhamisi asubuhi kuelekea kazini katika eneo la Bonde la Ufa, ambako alikagua ukarabati wa shule tano Elgeyo Marakwet. Pia alikuwa Turkana ambapo alikutana na kuzungumza na wanajeshi waliotumwa huko kabla ya kwenda Pokot Magharibi. Wakati wa ajali hii, Jenerali Ogolla na timu yake walikuwa wakielekea Kaunti ya Uasin Gishu. Kufuatia kifo cha Ogolla, Ruto ametangaza siku tatu za maombolezo huku bendera zikipepea nusu mlingoti. "Wakati huu wa maombolezo ya kitaifa, bendera ya Kenya, Bendera ya Jeshi la Ulinzi la Kenya, na bendera ya jumuiya ya Afrika Mashariki zitapepea nusu mlingoti katika balozi za Jamhuri ya Kenya na Kenya nje ya nchi," Ruto alisema. Uchunguzi umeanza kubaini kilichosababisha ajali hiyo. #mkuuwamajeshi #Jenerali #FrancisOgolla #rais #kenya #williamruto #ndege #jeshi #ajali #nairobi #voa #voaswahili
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Francis Ogolla Afariki katika Ajali ya Ndege
- 15 Jul 2025 - Spanish police have arrested nine people over rare anti-migrant unrest that rocked the town of Torre Pacheco, authorities said on Monday.
- 15 Jul 2025 - A nighttime fire at a nursing home has left nine people dead in the northeastern US state of Massachusetts after a desperate rescue operation, local authorities said Monday.
- 15 Jul 2025 - Karua, the People’s Liberation Party leader and long-time advocate for civil liberties, served as the chief guest at the cultural event that brought together members of the Kenyan diaspora in the U.S. Pacific Northwest.
- 15 Jul 2025 - In a statement released Monday, KUCO announced plans for mass demonstrations on Wednesday, July 17, in Nairobi. The union said it will present a public petition demanding immediate action to address what it described as the deteriorating state of public…
- 15 Jul 2025 - In a constitutional petition filed by UK-based activist Eliud Matindi, Justice Chacha Mwita ruled that there would be no interim orders preventing Lagat from carrying out his duties as Deputy Inspector General until the matter was fully heard and…
- 14 Jul 2025 - Mumias East Member of Parliament (MP) Peter Salasya has voiced concerns over the impending economic strain on Kenyan
- 14 Jul 2025 - Mumias East MP Peter Salasya has urged youths to actively participate in politics by vying for various elective
- 14 Jul 2025 - Human rights activist and Busia Senator Okiya Omtatah has sharply criticised President William Ruto’s recent directive to police
- 14 Jul 2025 - Interior Cabinet Secretary Kipchumba Murkomen has assured the nation that Kenya is fully prepared to host the 2025 CHAN tournament, with robust security arrangements firmly in place to guarantee the safety of teams, officials, and fans. Speaking after…
- 14 Jul 2025 - The Office of the Director of Public Prosecutions (ODPP) charged the suspects with committing a terrorist act contrary to Section 4(1) of the Prevention of Terrorism Act No. 30 of 2012.