Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alitoa wito kwa mateka wa Gaza kuachiliwa.

  • | VOA Swahili
    286 views
    Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell siku ya Alhamisi alitoa wito kwa mateka wa Gaza kuachiliwa mara moja, lakini akaiomba Israel "kutofanya maamuzi kwa hasira" katika vita vyake na wanamgambo wa Hamas katika ardhi ya Palestina. "Ninaelewa hofu na maumivu mliyonayo. Ninaelewa hofu na uchungu wa watu ambao wamevamiwa, kuchinjwa na kutekwa nyara. Naelewa hasira mlizonazo, lakini nikuombe msiendeshwe na hasira. Nadhani hivyo ndivyo nikiwa kama rafiki bora wa Israeli anaweza kukuambia."