Mkuu wa UN ayashinikiza mataifa kumaliza tofauti zao juu ya hatma ya vyanzo vya asili vya nishati

  • | VOA Swahili
    61 views
    Wakati Wanaharakati kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yakipinga pembeni mwa mkutano wa hali ya hewa, Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mkutano huo ameyashinikia mataifa siku ya Ijumaa kufikia makubaliano wakati mazungumzo yakianza tena, huku zikiwa zimebaki siku nne tu kwa mashauriano kuondoa tofauti zao juu ya hatima ya vyanzo vya asili vya nishati. Wakati mazungumzo ya Umoja wa Mataifa ni nadra kuamalizika kwa wakati, rais wa COP28 Sultan Al Jaber ameweka matarajio ya lengo ya kuhitimisha mkutano wa huko Dubai uwe ni saa tano asubuhi kwa saa huko siku ya Jumanne. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.