Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei asifia utendakazi wa polisi

  • | Citizen TV
    364 views

    Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei amesema kuwa maafisa wa usalama wa humu nchini wanatambulika kimataifa kutokana na ujasiri wao na mafunzo wanayopata ambayo yanawawezesha kukabiliana vilivyo na wahalifu. Kwenye mkutano na maafisa wakuu wa usalama hapa jijini Nairobi, Koskei amesema kuwa maafisa wa polisi wa humu nchini wana tajriba ya kutosha kukabili uhalifu nchini na katika mataifa ya nje.