Mlipuko wa volkano ulivyotokea Iceland

  • | BBC Swahili
    1,486 views
    Volkano imetokea kwenye rasi ya Reykjanes kusini-magharibi mwa Iceland baada ya wiki za matetemeko ya ardhi nchini humo. Picha zinaonesha lava ikipasuka kutoka kwenye volkano saa moja tu baada ya tetemeko la ardhi, au matukio ya tetemeko, kugunduliwa. Mlipuko huo ulianza kaskazini mwa mji wa Grindavik - kusini-magharibi mwa mji mkuu Reykjavik siku ya Jumatatu (18 Desemba), Ofisi ya Hali ya Hewa Iceland ilisema. #bbcswahili #iceland #tetemeko Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw