Mmiliki wa hospitali ya Mediheal Dkt Swarup Mishra ajitetea kuhusu tuhuma za biashara haramu ya figo

  • | Citizen TV
    156 views

    Mwanzilishi na mmiliki wa hospitali ya Mediheal Daktari Swarup Mishra ametupilia mbali ripoti ya kamati huru ya kuchunguza masuala ya biashara haramu ya figo nchini iliyopendekeza kuchungwa kwake zaidi kufuatia madai ya kuhusika kwa hospitali yake kwa biashara hiyo haramu. Mishra amekanusha madai hayo akisisitiza hospitali hiyo ilitoa huduma inavyopaswa kisheria kwa wagonjwa wote na kukosa kamati hiyo wakidai walifanya uchunguzi wao na lengo la kupata hospitali ya Mediheal na hatia.