Monica Juma na Raychelle Omamo wabadilisha wizara kwenye mageuzi serikalini

  • | Citizen TV
    Kwenye mabadiliko ya baraza la mawaziri Nafasi ya aliyekuwa waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri imechukuliwa na Peter Munya ambaye alikuwa katika wizara ya biashara na viwanda. Mutahi Kagwe ameteuliwa kuwa waziri wa afya huku Sicily Kariuki sasa akihamia wizara ya maji kutoka wizara ya afya. Betty Maina akiteuliwa kuhudumu katika wizara ya biashara na viwanda. Ukur Yattani ambaye amekuwa kaimu waziri wa hazina ya taifa sasa ataiongoza wizara hiyo. Aliyekuwa waziri wa ulinzi Raychelle Omamo wamebadilishana wadhifa na mwenzake wa masuala ya nchi za kigeni Monica Juma. Simon Chelugui amehamishwa kutoka wizara ya maji hadi ile ya leba .