Mpango wa Israel kukalia Gaza wapingwa.

  • | BBC Swahili
    2,303 views
    Baraza la mawaziri la Israel limeidhinisha pendekezo la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuidhibiti kwa ukamilifu na kukalia Ukanda wa Gaza. Hatua hii imepata pingamizi kutoka ndani na nje ya Israel. Kiongozi wa upinzani ametaja kama hatua ambayo inaathari kubwa kuliko manufaa kwa Israel huku Uingereza na Ujerumani zikikashifu vikali mpango huo. Marekani ambayo ni mshirika mkubwa wa Israel imesalia kimya kuhusu mpango huu ambao una uzito mkubwa hasa kwa misingi ya hatma ya mamilioni ya Wapalestina ambao wanaishi Gaza. @RoncliffeOdit anachambua kwa kina suala hili kwa pamoja na taarifa nyingine nyingi saa tatu usiku wa leo, mubashara kwenye Dira ya Dunia TV kupitia ukurasa wa YouTube, BBc Swahili. #bbcswahili #israel #gaza Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw