Mpango wa 'shamba system' unafikiriwa kuanzishiwa tena

  • | K24 Video
    51 views

    Mradi wa serikali wa kupanda miti bilioni 15 kufikia mwaka wa 2030 utaigharimu serikali takriban shilingi bilioni 600. Hata hivyo kulingana na kaimu mhifadhi mkuu wa misitu Alex Lemarkoko ,kutumia mfumo wa shamba system serikali itaweza kupunguza gharama hiyo kwa angalau asilimia hamsini. Kinachohitajika ni kuhakikisha mfumo huo utazingatia matakwa ya sheria na kuwa na usimamizi bora.