Skip to main content
Skip to main content

Mradi wa kawi kufaidi miradi ya maji kaunti za Kilifi na Mombasa

  • | Citizen TV
    143 views
    Duration: 2:00
    Licha ya madeni yanayosababisha uhaba wa maji katika kaunti za pwani, huenda wakazi wakapata afueni katika kaunti za Kilifi na Mombasa, kutokana na mradi wa nishati ya Jua inaolenga kupunguza gharama ya nguvu za umeme. Mradi huo unaoshirikisha Mamlaka ya kusambaza Maji Pwani Coast Kwa ushirikiano na Wizara ya Maji unafanyika katika eneo la Baricho eneo bunge la Malindi. Waziri wa Maji Eric Mugaa amesema mradi huo ambao umefika asilimia 90 ya ujenzi utapunguza kwa asilimia 20 nguvu za umeme zinatumika kusambaza Maji kaunti hizo. Mugaa amesema mamlaka hiyo hutimia takriban shilingi milioni 70 kila mwezi kulipia umeme.