Skip to main content
Skip to main content

Mradi wa ujenzi wa barabara nne muhimu kuanza

  • | Citizen TV
    2,695 views
    Duration: 1:55
    Mradi wa ujenzi wa barabara nne muhimu utakaogharimu takriban shilingi milioni 20 umezinduliwa mjini Malindi. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mbunge wa Malindi Amina Mnyazi amesema barabara hizo zitaimarisha usalama, kunadhifisha Mji pamoja na kurahisisha shughuli za usafiri. Chifu wa eneo hilo Wilfred Nyiro amesema endapo ujenzi huo utakamilika huenda ukabadili taswira ya Mji huo. Ujenzi wa barabara hizo unaotekelezwa na mamlaka ya KERRA unatarajiwa kusaidia maelfu ya wafanyibiashara haswa msimu wa mvua unapowadia.