- 11,798 viewsDuration: 2:45Msafara wa Kinara wa chama cha DCP Rigathi Gachagua kwa mara nyingine tena umevamiwa na wahuni katika Kaunti ya Nakuru. Shambulio hilo lilitokea katika eneo la Salgaa muda mfupi baada ya naibu huyo wa zamani wa rais kumtaka Rais William Ruto kukoma kumshambulia Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwa madai ya kuwa mdhamini wa upinzani. Gachagua amewataka wakazi wa Kaunti ya Nakuru kudumisha umoja.