Msafara wa M-Pesa Sokoni watua Elgeyo Marakwet

  • | Citizen TV
    267 views

    Msafara wa Mpesa Sokoni ulitua katika kitovu cha Kaunti ya Elgeyo Marakwet kwa ziara ya kwanza kabisa eneo hilo, ukizuru maeneo ya Chebara, Cheptongei, Kimnai, Kapcherop na Moiben. Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imeandaa ziara hii kwa lengo la kuwafikia wateja wake kwa ushirikiano na vituo vya Radio Citizen na Chamgei FM,vinavyomilikiwa na kampuni ya Royal Media Services, kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 18 ya huduma za MPESA nchini.