Msako wa kutafuta sumu iliyoibwa unaendelea Kiambu

  • | Citizen TV
    1,349 views

    Wizara ya afya inawataka watu walioiba mitungi ya kemikali yenye sumu aina ya sodium cyanide kutoka kwenye lori lililopinduka katika eneo la rironi kaunti ya Kiambu, kuisalimisha mara moja. Huku msako unaoshirikisha maafisa wa afya wa serikali kuu na kaunti ukiendelezwa katika nyumba eneo hilo, naibu mkurugenzi mkuu wa afya dkt sultani matendechero, amewaonya waliochukua mitungi hiyo kuwa ina sumu kali na ni hatari kwa maisha yao. pia wakazi wametahadharishwa kuhusu uwezekano wa kemikali hiyo kuvuja na kuenea katika maeneo yaliyoko karibu na eneo la tukio.