Skip to main content
Skip to main content

Mshikemshike waibuka Narok polisi wakizuia jaribio la kumtorosha mshukiwa wa mauaji

  • | Citizen TV
    1,005 views
    Hali ya mshikemshike ilishuhudiwa nje ya mahakama ya Narok hii leo, polisi walipokabiliana kwa risasi na vitoa machozi na kundi la watu waliokuwa wakitaka kumtorosha mshukiwa wa mauaji. Zogo hilo lilizuka baada ya mahakama kuahirisha kesi ili mshukiwa afanyiwe uchunguzi wa akili. Mamia ya wafuasi wa jamaa huyo waliokuwa wamezuiwa na polisi nje ya mahakama, walijaribu kumnasua mshukiwa huyo na kusababisha makabiliano makali