Mshukiwa ukabaji wa Magadi afikishwa mahakamani kaunti ya Kajiado

  • | Citizen TV
    595 views

    Mshukiwa wa ubakaji eneo la Magadi kaunti ya Kajiado Nkondio Sakoi amefikishwa mahakamani leo na kukabiliwa na mashtaka ya ubakaji. Sakoi anatuhumiwa kumbaka mwanamke mmoja eneo la Oloika, Magadi. Mahakama imeamrisha aachiliwe kwa dhamana ya shilingi laki tano, huku hofu ikiendelea kugubika eneo hili ambako wanawake 7 wameripoti kubakwa.