Skip to main content
Skip to main content

Mtaala wa elimu ya ufundi waongeza muda wa kuhitimu hadi miezi sita kutoka mitatu

  • | Citizen TV
    181 views
    Duration: 1:13
    Ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaohitimu kutoka vyuo vya ufundi nchini wana ujuzi wa kutosha kupata ajira nchini na hata ughaibuni kwa urahisi, serikali imetangaza kuongezwa kwa muda wa mwanafunzi yeyote kuhitimu kutoka miezi mitatu hadi sita. Akizungumza alipofungua kongamano la kujadili Mbinu za kuboresha mtaala wa vyuo vya ufundi mjini Nyeri, Katibu wa elimu ya ufundi Esther Mworia, ameeleza kuwa hatua hiyo imechukuliwa kuhakikisha mahafala wa vyuo hivyo wanahitimu kwa ujuzi na uzoefu unaohitajika na waajiri.