Mtihani wa KCSE Waanza, Shule ya Merishaw yafanya kwa mara ya Kwanza

  • | Citizen TV
    1,061 views

    Huku Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) ukianza rasmi kote nchini, wanafunzi 52 kutoka Shule ya Merishaw iliyoko Isinya, Kaunti ya Kajiado, wanaufanya mtihani huo kwa mara ya kwanza.

    Wanafunzi na walimu wameonyesha imani kubwa, wakilenga kuweka viwango vya juu kwa watahiniwa wa baadaye katika shule hiyo.

    Wanafunzi hawa ni miongoni mwa watahiniwa 14,058 wanaofanya mtihani wa KCSE katika vituo 166 kwenye Kaunti ya Kajiado. Idara ya Elimu ya Kaunti hiyo imeripoti kuwa mtihani umeanza vizuri bila changamoto yoyote kwenye vituo vyote.