Mtoto afariki baada ya nyumba kuteketea moto Kikuyu

  • | Citizen TV
    531 views

    Mtu mmoja amefariki huku wengine 30 wakiachwa bila makao baada ya moto kuteketeza makaazi yao katika kijiji cha Reli eneobunge la Kikuyu kaunti ya Kiambu. Moto uliripotiwa kijijini humo usiku wa kuamkia leo, ambapo nyumba 18 ziliteketezwa. Aliyefariki ni mtoto wa miaka mitatu. Aidha wakaazi wanaripoti kupoteza mali ya thamani isiyojulikana. Waathiriwa wamelaumu maafisa wazima moto kutoka kaunti ya Kiambu kwa kuchelewa kushghulikia dharura. Uchunguzi wa chanzo cha moto huo umeanzishwa