Mtoto mdogo aongoza ibada ya kumbukumbu kwa marehemu Brazil.

  • | BBC Swahili
    1,870 views
    Video ya mtoto mdogo akiongoza ibada ya kitamaduni pamoja na wazee wake imeenea sana nchini Brazil. Walama Aris, mwenye umri wa mwaka 1 na miezi 7 pekee, alishiriki katika mila hiyo ya kale ya jamii za kiasili katika eneo la Xingu, mkoani Mato Grosso, jimbo lililopo magharibi mwa Brazil na ambalo sehemu kubwa limefunikwa na msitu wa Amazon. Kwa mujibu wa wazazi wake, hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Walama kushiriki katika sherehe hiyo ya siku saba ya kuwaenzi ndugu waliofariki dunia. #bbcswahili #brazil #utamaduni Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw