- 550 viewsTangu kuanza kwa vita huko Gaza, Abdel Jaber Mohammed al-Farra alisema amepoteza vitu vingi – makazi yake, ujirani wake na shule yake. Farra na familia yake walikimbia makazi yao katikaujirani wa al-Manara upande wa mashariki ya Khan Younis baada ya majeshi ya Israeli kupiga bomu jengo. “Eneo tunaloishi liko salama, lina msikiti, ambako jina la Mungu linatukuzwa. Hakuna kitu, sote ni watu wa amani, hakuna kitu kibaya chochote katika ujirani wa al-Manara, ni salama na kimya, na eneo liko wazi,” alisema baba wa Abdel Jaber, Mohammed. Baada ya kushindwa kupata sehemu katika shule ambayo tayari imefurika watu waliokoseshwa makazi katika eneo, familia hiyo imekuwa ikiishi usiku kucha kila siku nje ya shule kwenye vibaraza. “Tuliweka vichwa vyetu chini na kujifunika na taulo, hadi asubuhi ilipoingia,” alisema Abdel Jaber. “Hali ni ya msiba mkubwa. Tunayaomba mataifa yote kututumia misaada, kufungua kivuko cha mpakani cha Rafah, ili kuleta misaada, na kumaliza vita. Malizeni hii dhulma dhidi yetu. Nyumba zetu zote zimepigwa mabomu,” alisema mtoto huyo wa miaka nane. Majeshi ya Ulinzi ya Israel yamekuwa yakipiga mabomu katika eneo la Palestina tangu uvamizi wa Hamas wa mashambulizi ya kuvuka mpaka ya Oktoba 7 ambapo maafisa wa Israeli wanasema watu 1,200 waliuwawa. Mashambulizi ya Israeli yameua zaidi ya Wapalestina 23,000, kuharibu sehemu kubwa ya Gaza na kuwakosesha makazi wengi angalau kati ya watu milioni 2.3, ikileta hali ya taharuki na mgogoro mbaya sana wa kibinadamu. - Reuters #Haifa #waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera
Mtoto wa Kipalestina miaka nane aeleza madhila yanayo wakabili
- 14 Aug 2025 - At least 22 migrants died after two boats overturned in the Mediterranean on Wednesday, with more still missing and some 60 survivors, humanitarian agencies said.
- 14 Aug 2025 - The summit between US President Donald Trump and his Russian counterpart Vladimir Putin will be held at Joint Base Elmendorf-Richardson in Alaska, a White House official said Wednesday.
- 14 Aug 2025 - Only Ukrainian President Volodymyr Zelensky can negotiate a land deal with Russia in an effort to end Moscow's war against his country, French President Emmanuel Macron said on Wednesday.
- 14 Aug 2025 - South Africa's unemployment rate rose for the second quarter in a row, official data showed on Tuesday, highlighting one of the biggest challenges faced by the country's year-old coalition government.
- 14 Aug 2025 - Workers at the Kenya Pipeline Company (KPC) are demanding job security assurances as the government moves to sell a majority stake in the State corporation.
- 14 Aug 2025 - "Parliament must be called out. Something is going on in our Legislature that we must address. Money is being demanded from the Executive, governors, and ministers—especially those who appear before parliamentary committees for accountability,” said…
- 14 Aug 2025 - The Kenya National Commission on Human Rights (KNCHR) wants victims of protests and demonstrations to receive more than just monetary compensation.
- 14 Aug 2025 - Kenyan exports set for battle against Team Kenya stars once again
- 14 Aug 2025 - Lack of electricity delays handing-over of Gichugu housing project
- 14 Aug 2025 - Housing to remain key at World Urban Forum