Maiti ya msichana wa miaka 7 imepatikana ikiwa uchi katika kijiji cha Mwezang’ombe, eneo bunge la Kilifi North, kaunti ya Kilifi, baada ya mtoto huyo kuripotiwa kupotea Jumapili jioni alipokuwa akicheza nyumbani. Kulingana na mamake, alimwona mwanawe kwa mara ya mwisho aliporudi nyumbani kunywa maji kabla ya kuondoka tena na baadaye kutoweka bila kujulikana alipoenda.
Juhudi za familia kumtafuta hadi usiku wa saa nane hazikufua dafu, lakini walipoendeleza msako asubuhi walimkuta mtoto huyo akiwa ameuawa kikatili. Ripoti ya awali ya uchunguzi imebaini kuwa alinyongwa, shingo kuvunjwa na kisha kunajisiwa, huku familia ikidai haki na viongozi wa usalama wakiahidi kuchunguza tukio hilo na kuwakamata waliohusika