- 9,310 viewsDuration: 2:34Familia moja eneo la Sagana, Kaunti ya Kirinyaga, inaendelea kumtafuta mtoto wao wa miaka sita aliyetoweka baada ya kutoka shuleni Jumatatu wiki hii. Shantel Nekesa alinaswa kwenye kanda ya video katika kijiji chao akiwa na mwanamume ambaye hadi sasa hajatambuliwa. Tukio hilo linajiri siku chache baada ya Wizara ya Jinsia na Watoto kutoa tahadhari kuhusu kuongezeka kwa visa vya watoto kutoweka nchini.