- 1,368 viewsDuration: 1:20Mtu mmoja amefariki huku wengine watatu wakiokolewa kwenye vifusi vya jengo la ghorofa tatu lililoporomoka katika kijiji cha Motoa Wadi ya Kipchebor, Kaunti ya Kericho. Waziri wa Utumishi wa Umma kaunti ya kericho Jonathan Korir aliongoza shughuli za uokoaji, kuratibu juhudi kati ya wahudumu wa dharura na waliojitolea katika eneo la tukio. Watu watatu walionusurika walipelekwa katika vituo vya afya vilivyo karibu kwa matibabu,. Bado haijulikani kilichosababisha jengo hilo kuporomoka.