- 3,092 viewsDuration: 1:52Mtu mmoja amefariki huku wengine 8 wakijeruhiwa baada ya mchanga kuporomoka kwenye mgodi wa dhahabu na kuwafunika katika kijiji cha Maclif eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega. Majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya misheni ya mukumu baada ya kuokolewa. Kutokana na mkasa huo Wachimba mgodi wenye hamaki walivamia timbo jirani na kuiteketeza kwa madai kwamba walisababisha mchanga huo kuporomoka kwa kulipua baruti.