Mtu mmoja auwawa kwenye maandamano Kakamega

  • | Citizen TV
    6,765 views

    Mtu mmoja ameaga dunia baada ya kupigwa risasi wakati wa maandamano dhidi ya serikali katika kaunti ya Kakamega. Mwanaume huyo alipigwa risasi wakati polisi walijaribu kumuokoa mwenzao anayedaiwa kupokonywa bunduki na baadhi ya waandamanaji. Haya yanajiri huku watu wengine wanne wakijeruhiwa katika kaunti za Kisumu na Mombasa. Laura Otieno na taswira kamili ya maandamano ya Jumanne.