Mtu mwenye umri mdogo zaidi duniani kutumia miguu ya bandia yenye mfumo wa kompyuta

  • | BBC Swahili
    444 views
    Harmonie-Rose, mwenye umri wa miaka nane kutoka Bath, nchini Uingereza, alikatwa viungo vyake vyote baada ya kupata homa ya uti wa mgongo alipokuwa mtoto. Sasa, amekuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi duniani kuwekewa miguu ya bandia yenye microprocessor, Kompyuta ya ndani inayofuatilia mienendo yake kila wakati na kufanya marekebisho ambayo yanamruhusu kutembea na kukaa. #bbcswahili #uingereza #ulemavu