Mudavadi apuzilia madai kuhusu uhusiano wa Kenya na Marekani

  • | Citizen TV
    820 views

    Waziri wa Masuala ya kigeni Musalia Mudavadi amepuuzilia mbali madai kuwa uhusiano kati ya Kenya na Marekani unayumba, kufuatia mswada uliowasilishwa katika bunge la Congress na Seneta James Risch wa Marekani. Risch anapendekeza Kenya ipokonywe hadhi yake ya mshirika asiye mwanachama wa NATO akitaja hatua ya Kenya kujihusisha zaidi na Uchina, na tuhuma za kushirikiana na kundi la waasi wa RSF nchini Sudan.Mudavadi anasisitiza mswada huo sio msimamo wa serikali ya Marekani, akisisitiza uhusiano wa Nairobi na Washington unasalia imara.