Mudavadi: Kufurushwa kwa Karua kutoka Tanzania kulizingatia sheria

  • | KBC Video
    5,064 views

    Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi amedai kwamba viongozi wa upinzani akiwemo kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, wanachelewesha mchakato wa usaili wa makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kwa kuiomba mahakama kuu kupitia mawakala wao kusitisha shughuli hiyo. Mudavadi ambaye pia ni waziri wa mashauri ya nchi za kigeni pia hakumsaza Martha Karua na washirika wake waliorejeshwa kutoka nchini Tanzania, akisema walishughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo. Mudavadi alizungumza wakati wa hafla ya mazishi huko Malava, kaunti ya Kakamega.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive