Waziri wa usalama wa taifa Kipchumba Murkomen amepuzilia mbali madai kwamba asasi za usalama zilihusika kwenye shambulizi lililotokea kanisani huko Witima, eneo bunge la Othaya, kaunti ya Nyeri. Murkomen alisema siyo desturi au sera ya serikali kuvuruga maabadi, akisema uchunguzi unaendelea kubaini wale waliotekeleza vitendo hivyo vya kuchukiza. Akizungumza kwenye mkutano ulioandaliwa na spika wa bunge la kitaifa, Murkomen alikashifu wanasisa wanaohudhuria mikutano ya kanisa wakiandamana na wahuni waliojihami.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive