- 1,559 viewsDuration: 2:58Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen ameendeleza msimamo wake kuwa hakuna makosa kwa wakenya kuwapa maafisa wa polisi mafuta wanapohitaji, ili kufanikisha usalama kwa wananchi. Murkomen akionekana kuwakosoa wale anaosema wanakerwa na matamshi yake. Alizungumza kaunti ya Mandera ambako pia ametangaza kuwa machifu eneo hilo watapewa silaha na mafunzo maalum ya kijeshi kujilinda na mashambulizi ya mara kwa mara ya Al Shabaab.