MUSEVENI AONYA MATAIFA YA NJE KUTOINGILIA SIASA ZA UGANDA

  • | VOA Swahili
    Rais mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameonya mataifa ya kimataifa dhidi ya kuingilia masuala ya ndani ya Uganda huku akiutaja upinzani nchini humo kuwa vibaraka wa wazungu. Dkt Kizza Besigye, mpinzani wake wa miaka mingi nchini humo amemjibu Museveni kwa kueleza kuwa raia wa Uganda wana uhuru wa kutangamana na yeyote. Kama anavyoripoti Mwandishi wetu wa Kampala, Kennedy Wandera, mpinzani wake wa karibu Bobi Wine angali amezuiliwa ndani ya nyumba yake na majeshi.