Muungano unaopendelea demokrasia wasaini mkataba wa serikali ya mpito ya kiraia

  • | VOA Swahili
    62 views
    Ushirika unaounga mkono demokrasia nchini Sudan wa Forces of Freedom and Change umesaini makubaliano ya awali na jeshi ili kurejesha utawala wa kiraia baada ya mapinduzi ya mwaka jana. Makubaliano haya yanaruhusu uongozi wa mpito wa kiraia wa miaka miwili kuelekea uchaguzi mkuu. Lakini maandamano ya kupinga makubaliano hayo yameanza katika mji mkuu, Khartoum, na mengine zaidi yanatarajiwa nchi nzima, huku watu wakitaka wale walioongoza mapinduzi wawajibishwe. Sudan imeingia katika ukosefu wa uthabiti wa kisiasa kwa karibu miaka minne baada ya rais Omar al-Bashir kuondolewa madarakani kufuatia maandamano ya umma. - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.